Maoni ya viongozi kuhusu kubanduliwa kwa Gachagua

  • | Citizen TV
    7,407 views

    Viongozi mbalimbali kote nchini wametoa hisia mseto kuhusu kubanduliwa kwa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua tangu kutimuliwa kwake usiku wa kuamkia ijumaa. Viongozi wa karibu wa Gachagua wakishindwa kuhimili hisia zao na kutokwa na machozi wakidai kutimuliwa kwake ni njama ya kisiasa, ila baadhi ya viongozi wameunga mkono hatua ya kubanduliwa kwake wakidai kauli zake ndizo zilimponza .