Gachagua adai Rais Ruto amemfanyia ukatili mkubwa

  • | Citizen TV
    22,896 views

    Naibu rais aliyebanduliwa Rigathi Gachagua sasa anasema maisha yake na familia yake yako hatarini, akidai kuponea mara mbili njama za kuuawa kwa sumu. Akizungumza pindi tu alipotoka hospitali alikolazwa tangu siku ya alhamisi, Gachagua ametoa taarifa iliyosheheni kile amekitaja kuwa usaliti na ukatili kutoka kwa Rais William Ruto. Na kama Seth Olale anavyoarifu, Gachagua pia ameelezea kwa mapana masaibu yake yalipoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita