Laana ya kiti cha naibu rais nchini Kenya

  • | K24 Video
    1,788 views

    Kwa miongo kadhaa, ofisi ya naibu rais ukipenda makamu wa rais imekuwa ikishuhudia migogoro, vita vya kisiasa, hali ya kutoelewana na hata kutiliana shaka. Kutoka kwa makamu wa rais wa kwanza wa Kenya, Jaramogi Oginga Odinga, hadi kwa naibu rais wa sasa, Rigathi Gachgua, ofisi imeonekana kuwa na kama laana fulani kwa ukosefu wa maelewano kati ya rais na msaidizi wake. Je ofisi hiyo ni ya laana hapa kenya?