Wakenya waonywa kuhusu rangi iliyo na madini ya risasi

  • | KBC Video
    48 views

    Umma umetahadharishwa dhidi ya kununua rangi ambazo hazijafikia viwango vilivyowekwa na serikali na ambazo zinaweza kuwasababishia madhara ya sumu ya risasi au lead. Akizungumza jijini Nairobi wakati wa maadhimisho ya wiki ya kuzuia madhara ya sumu ya risasi, katibu katika idara ya afya ya umma Mary Muthoni alisema kituo cha kushughulikia haki kwa mazingira na maendeleo, CEJAD, alisema kwamba rangi zilizotengenezewa humu nchini katika miaka ya 2013, 2019 na 2021, zilikuwa na kiwango kikubwa cha risasi. Muthoni aliongeza kuwa athari zinazotokana na sumu ya risasi ni kama vile matatizo ya kiakili kwa watoto na utasa au mimba kuharibika miongoni mwa wanawake wajawazito. Alitoa wito kwa uchunguzi wa mapema ili kubaini viwango vya sumu ya risasi katika damu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive