Wakazi wa Homa Bay wapokea huduma za matibabu

  • | KBC Video
    6 views

    Takriban wakazi elfu tatu wa kaunti ya Homa Bay walipokea huduma za matibabu bila malipo kufuatia ufadhili wa wakfu wa Safaricom kwa ushirikiano na hospitali ya Zuri Health, wakfu wa Amref na wadau wengine.Meneja wa mipango wa Wakfu wa Safaricom, Sophy Onyango alisema lengo la kambi hiyo ya matibabu bila malipo ni kuhamasisha umma kuhusu magonjwa kama vile nasuri, saratani na shinikizo la damu miongoni mwa wakazi. Afisa mkuu wa afya katika kaunti ya Homa Bay Kevin Osuri, aliwashauri wakazi kujisajili kwa mpango wa halmshauri ya afya ya jamii ili waweze kumudu gharama ya matibabu katika vituo vya afya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive