Serikali yahimizwa kuzingatia ushahidi kukomesha mrundiko mahakamani

  • | KBC Video
    72 views

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu katika kaunti ya Mombasa yametoa wito kwa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutathmini kwa makini kesi zinazowasilishwa mahakamani kuhakikisha kwamba ni zile zinazostahili pekee zinazoshughulikiwa. Makundi hayo yanasema kufanya hivyo kutapunguza mrundiko wa kesi mahakamani na matumizi mabaya ya rasilimali. Wakiongea kufuatia kuachiliwa huru kwa washukiwa 14 waliokamatwa wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, viongozi wa makundi hayo wakiongozwa na Zedekiah Adika walihimiza mahakama kuwa na utaratibu madhubuti wa kudumisha kesi mahakamani. Adika alisema kesi zisizokuwa na ushahidi wa kutosha husababisha mrundiko na kuzipotezea mahakama muda mwingi mbali na kugharimu kiasi kikubwa cha pesa

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive