Hoja ya kumbandua linturi yaungwa mkono na wabunge 149 huku 36 wakipinga kuondolewa kwake

  • | K24 Video
    84 views

    Wabunge kumi na mmoja wakiwemo TJ Kajwang, George Murugura, Robert Mbui, na Naomi Waqo wameteuliwa na kuidhinishwa na bunge kuwa katika kamati maalum inayochunguza sababu za kutaka Mithika linturi ang'atuliwe kama waziri wa kilimo. Hoja ya kumbandua linturi iliungwa mkono na wabunge mia moja arobaini na tisa huku thelathini na sita pekee wakipinga kuondolewa kwake kufuatia sakata inayoandama wizara ya kilimo ya mbolea ghushi. Kikao cha bunge hii leo kilikuwa na mjadala mkali kuhusu hoja hiyo.