Vurugu Yazuka Mazishini Kirinyaga, Wamumbi Ashambuliwa na Vijana

  • | K24 Video
    214 views

    Kulikuwapo na taharuki leo wakati wa mazishi katika kijiji cha Muragara, eneo bunge la Ndia, Kaunti ya Kirinyaga, baada ya Mbunge wa Mathira, Eric Wamumbi, kushambuliwa na kundi la vijana alipokuwa akihutubu.Inadaiwa kwamba vijana hao walikasirishwa na matamshi ya Wamumbi kumhusu aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, wakidai alimtaja vibaya mbele ya waombolezaji.