Kesi ya kuzuia kuapishwa kwa naibu rais mwingine yawasilishwa katika mahakama kuu ya Eldoret

  • | K24 Video
    58 views

    Kesi ya kuzuia kuapishwa kwa naibu rais mwingine endapo Rigathi Gachagua ataondolewa ofisini na bunge la seneti imewasilishwa katika mahakama kuu ya Eldoret. Wakili morara omoke amefanya ombi la kumruhusu Gachagua kuhudumu kama naibu rais hadi pale kesi zote zinazohusiana na kubanduliwa kwake zisikizwe na kuamuliwa na mahakama. Kigezo ambacho wanaomtaka Gachagua kuondoka huenda wakakabiliana nacho.