Nafasi ya katibu wa wizara ya jumuiya ya Afrika Mashariki

  • | K24 Video
    7 views

    Wakenya mia moja na tisa pekee wamefaulu kuwa miongoni watakaohojiwa na tume ya kuajiri wafanyikazi wa umma PSC kati ya elfu mbili mia tano kumi na saba walioomba kujaza nafasi ya katibu wa wizara ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Miongoni wa walioorodheshwa ni aliyekuwa gavana wa Nairobi Anne Kananu, aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha walimu KNUT wilson sossion na mwanablogu maarufu Gabriel Oguda . Utata unaibuka kuhusu iwapo walioorodheshwa ni wa kujaza nafasi moja tu au huenda mabadiliko yakashuhudiwa katika nafasi za makatibu katika wizara tofauti.