Rais Ruto afanya kikao hii leo na viongozi wa makanisa ya kiivanjilisti katika ikulu ya Nairobi

  • | K24 Video
    6 views

    Rais William Ruto amefanya kikao hii leo na viongozi wa makanisa ya kiivanjilisti katika ikulu ya Nairobi kwa kile kinachoonekana kama kujaribu kurejesha uhusiano bora baina ya serikali yake na viongozi wa dini. Katika siku za hivi majuzi, viongozi wa makanisa wamekuwa wakiikosoa serikali ya rais Ruto kuhusiana na maswala tofauti yanayoathiri wakenya na taifa kwa ujumla. Ruto aliyepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa makanisa katika uchaguzi uliopita amejipata katikati ya shutuma kutoka kwa viongozi hao