Wanasiasa 14 wakamatwa kuhusiana na visa vya wizi wa mifugo katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya

  • | K24 Video
    23 views

    Wanasiasa 14 wamekamatwa kuhusiana na visa vya wizi wa mifugo katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya wakati wa operesheni ya maliza uhalifu ambayo imedumu kwa takribani miaka miwili sasa. Visa vya wizi wa mifugo katika maeneo hayo vimepungua huku kwa zaidi ya bunduki 100 zikipatikana. Hata hivyo shule 13 bado zimesalia kufungwa katika kaunti za Baringo ,Pokot magharibi na Turkana kutokana na ukosefu wa usalama.