Hoja ya kubanduliwa ya Rigathi Gachagua

  • | K24 Video
    238 views

    Naibu rais aliyebanduliwa Rigathi Gachagua sasa anataka uchunguzi kuhusu ni vipi kesi iliyompa afueni ya kusalia afisini iliyokuwa mbele ya jaji Chacha Mwita imeanza ghafla kushughulikiwa na jopo la majaji watatu bila ya idhini ya jaji mkuu Martha Komme. Gachagua anadai kuwa huenda ni njama ya kumuapisha naiba rais mtarajiwa Kithure Kindiki hapo kesho siku ambayo jopo hilo litatoa mwelekeo kuhusu kesi ya Gachagua.