Afueni ya maji Malindi

  • | Citizen TV
    269 views

    Ni afueni kwa wakaazi wa malindi kaunti ya kilifi baada ya kubainika kuwa uhaba wa maji umepungua kwa asilimia 30. Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya maji ya malindi Felix wanje, ambaye amedokeza kuwa mradi wa baricho-kakuyuni uliozinduliwa hivi maajuzi umewapa wakaazi afueni. Kwa sasa wakaazi hao wanasema kuwa tatizo la uhaba wa maji limepata suluhu baada ya ukarabati wa bomba kubwa la kusambaza maji kutoka kituo kikuu cha Baricho -Kayuni hadi malindi kukamilika.