Ajira Ughaibuni I Mashirika 20 yapokonywa leseni kwa kuwalaghai Wakenya

  • | KBC Video
    34 views

    Serikali imefutilia mbali leseni za mashirika 20 ya uajiri watu kwa madai ya kuwalaghai wakenya wakiwaahidia nafasi za kazi zisizokuwepo. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu mashauri ya nchi za kigeni na maslahi ya wakenya walio ughaibuni, mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya kitaifa ya masuala ya ajira Edith Okoki alisema baadhi ya kampuni zilizofungwa zilijaribu kujisajili upya kwa kutumia majina mapya lakini zikaripotiwa. Halmashauri hiyo, bila kutaja majina ya mashirika hayo, ilisema kuwa wanasiasa kadhaa walikuwa wakijaribu kulinda mashirika hayo yanayoendeleza shughuli za kilaghai.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive