Amani ya muda imeonekana kurejea bonde la ufa kufuatia oparesheni ya maofisa wa polisi

  • | Citizen TV
    2,420 views

    Kufuatia operesheni Maliza Uhalifu inayoendeshwa na serikali kaskazini mwa bonde la ufa, amani ya muda imeonekana kurejea katika maeneo yaliyoshuhudia visa vingi vya uhalifu, jamii zikianza kukumbatiana na kuishi kwa amani. Hata hivyo Kuna uwezekano wa amani hiYo kutodumu iwapo serikali haitaweka mbinu za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ambayo mara nyingi huwa chanzo cha jamii hizo kupigania malisho.