Ashura: Igizo la vita vya Kerbala na kifo cha Imam Hussein

  • | VOA Swahili
    140 views
    Maelfu ya Wairan wameadhimisha siku ya Ashura Jumanne (Julai 16), sikukuu ya kidini ya kumuenzi Imam Hussein aliyekufa shahidi, ambaye ni mjukuu wa Mtume Muhammad. Ashura, ni maadhimisho ya kila mwaka ambapo watu huonyesha michezo yenye kuvutia na kuigiza Vita vya Kerbala ambavyo Imam Hussein alifariki, inafanyika katika siku ya kumi ya mwezi wa Muharram, mwezi wa kwanza wa kalenda ya Kiislam. Waislam wa madhehebu ya Shia waliandamana mitaani wakifanya maigizo, kuchoma hema ikiwa ni ishara ya kuigiza shida alizozipata Imam Hussein, na kupaza sauti wakiomba. “Kulingana na mazingira ya Wapalestina na Gaza, na matukio yanayofanyika hivi sasa, kuwatetea watu wasiokuwa na hatia ni ujumbe muhimu zaidi unaotakiwa kupelekwa kote,” alisema moja wa waumini Bi Mortazavi. Vita hiyo viligawanya madhehebu ya Shia na Sunni. -Reuters #wairan #iran #kerbala #maadhimisho #muharam #ashura #imamhussein #voa #voaswahili