Marehemu askofu mstaafu wa kanisa katoliki Philip Sulumeti alizikwa leo katika kaunti ya Kakamega huku waombolezaji wakimkumbuka kwa wajibu wake wa kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu na mfumo wa utoaji huduma za matibabu nchini. Mazishi hayo yalihudhuriwa na familia, marafiki, viongozi wa kidini na maafisa wa ngazi za juu serikalini wakiongozwa na waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi. Mudavadi akitambua mchango wake kupitia uzinduzi wa shule na vituo kadhaa vya afya alitaja mazishi yake kuwa adhimu japo buriani kwa mja aliyekuwa na imani thabiti.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive