Athari ya ushuru wa Trump kwa mataifa ya kigeni

  • | BBC Swahili
    1,969 views
    Canada na Mexico zimetangaza ushuru kwa bidhaa za Marekani, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa nchi hiyo, baada ya ushuru wa asilimia 25 wa Washington kwa nchi hizo mbili kuanza kutekelezwa Jumanne. Waziri wa Biashara wa Marekani Howard Lutnick amesema kuwa Rais Trump pengine atatangaza mpango wa kupunguza ushuru kwa Canada na Mexico. Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada ameiambia BBC ofisi yake haijapata taarifa kuhusiana na mpango huo.