Athari za mabadiliko ya tabianchi na utashi wa binadamu

  • | K24 Video
    85 views

    Kuna hofu ya viumbe wengi baharini kuwa katika hatari ya kuangamia kutokana na uharibifu wa mazingira ya viumbe hao pamoja na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa viumbe hao ni kasa ambao idadi yao imeendelea kupungua kwa kasi kubwa. Uvuvi haramu unaosababishwa na utashi mkubwa wa nyama ya kasa, mayai yake pamoja na mafuta kumemuweka kasa katika hatari hiyo.