Baraza la viongozi wa Kiislamu laandaa kongamano la amani

  • | KBC Video
    63 views

    Baadhi ya viongozi wa kidini wanasema watu binafsi na mashirika yanapaswa kuwasilisha suluhu zenye msingi wa imani ili kukabiliana na itikadi kali na kutetea amani, mazungumzo na kuishi pamoja duniani. Matamshi hayo yalitolewa leo wakati wa kongamano lenye kauli mbiu uislamu na amani lililoandaliwa katika kituo cha Iran Cultural Centre jijini Nairobi. Wanenaji kwenye mkutano huo walielezea masuala muhimu ambayo ni pamoja na amani ulimwenguni kutoka mtazamo wa kislamu, mazungumzo ya dini mbalimbali na jukumu la uislamu katika kutatua mizozo katika karne ya ishirini na moja.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive