Bei ya petroli yatarajiwa kuongezeka

  • | KBC Video
    88 views

    Huenda bei ya mafuta ya petroli ikaongezeka iwapo halmashauri ya kudhibiti kawi humu nchini itaanza kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya pili ya utafiti kuhusu bei ya bidhaa hizo humu nchini. Iwapo yatatekelezwa, bei ya petroli itaongezeka kwa shilingi saba na senti 80, ile ya dizeli kwa shilingi saba na senti sabini na tano huku lita moja ya mafuta ya taa ikiuzwa kwa shilingi saba na senti sitini na saba. Mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyo Daniel Kiptoo amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wauzaji bidhaa hizo wanapata faida huku wakiendelea kuwekeza kwenye muundo mbinu na huduma bora.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive