Bodi ya elimu ya juu nchini yachunguza shahada za digrii za hadhi zilizokabidhiwa Oscar Sudi

  • | Citizen TV
    385 views

    Bodi ya elimu ya juu nchini sasa inasema inachunguza shahada za digrii za hadhi zilizokabidhiwa baadhi ya wabunge kadhaa juma lililopita. Uchunguzi huu unafuatia kutuzwa kwa wabunge Oscar Sudi wa Kapseret, mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa na John Waluke wa Sirisia na shahada za digrii za hadhi za chuo kikuu cha Northwestern Christian University. Bodi hii sasa ikisema kuwa chuo hicho hakijaidhinishwa kuendesha shughuli zake za elimu na hivyo basi vyeti vyake havitambuliki hapa nchini.