Bodi ya madaktari wa mifugo kuanza kutoa chanjo

  • | Citizen TV
    213 views

    Rais William Ruto, anapoendelea kuwasuta wale wanaoendeleza pingamizi na upinzani dhidi ya mpango wa chanjo ya mifugo inayonuiwa kufanikishwa mapema mwakani, bodi ya madaktari wa mifugo nchini KVB imevunja kimya Chake. Afisa Mkuu mtendaji wa bodi hiyo Dkt.Mary Agutu akielezea utayari wa bodi katika kufanikisha chanjo ya mifugo kote nchini. Hatua hiyo inazidi kuibua hisia mseto kama anavyoarifu Mwanahabari wetu Bonface Barasa kutoka Kaunti ya Isiolo.