Bodi ya Utalii nchini yapanga safari ya siku tano kama njia ya kupiga jeki utalii wa michezo

  • | Citizen TV
    387 views

    Bodi ya Utalii nchini Kenya imezindua safari ya siku tano ya urithi inayoanza katika kaunti ya Laikipia na itamalizika katika kaunti ya Nandi siku ya Jumamosi. Safari hiyo ya mashindano ya riadha na kuendesha baisikeli itapitia kaunti za Elgeyo Marakwet, Baringo na Uasin Gishu. KTB imeanzisha mradi huu kama njia ya kukumbatia utalii wa michezo na pia kuwapa watalii wa ndani na wa kimataifa chaguzi zaidi isipokuwa uzoefu wa jadi wa utalii wa pwani na pori. Mfululizo huo unajumuisha hafla tano za michezo zilizoundwa kuonyesha uzuri na urithi wa kitamaduni wa Kenya. KTB imeshirikiana na shirikisho la riadha Kenya katika mradi huu na kilele kitakuwa mashindano ya kukimbia mlimani ya Bargetuny Jumamosi huko Tinderet, kaunti ya Nandi. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Utalii na Wanyama Pori Rebecca Miano, gavana wa Laikipia Joshua Irungu, na Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri, Felix Kosgey.