Skip to main content
Skip to main content

Bunge ladaiwa kudhoofisha ugatuzi

  • | KBC Video
    75 views
    Duration: 4:34
    Bunge la Kitaifa limekosolewa kwa madai ya kupiku majukumu yake na kudhoofisha ugatuzi, kufuatia kupunguzwa kwa mgao kwa serikali za kaunti kwa shilingi bilioni 23 katika mwaka wa kifedha wa 2025/26. hapo awali bunge la seneti lilipendekeza kutengwa kwa shilingi bilioni 93.5 kufadhili shughuli za serikali za kaunti zinazohusiana na ugatuzi, kabla ya Bunge la Kitaifa kupunguza fedha hizo hadi shilingi bilioni 70.66 wakati mswada ulipowasilishwa bungeni.Kupunguzwa kwa fedha hizo , ambako baadaye kuliidhinishwa na Kamati ya bunge la Seneti ya Fedha na Bajeti, kumekosolewa huku maseneta wakisema hakukuwa na uhalali wowote wa kufanya hivyo na kwamba hatua hiyo inahatarisha mwelekeo wa jinsi mabunge hayo mawili yatakavyoshughulikia masuala yanayohusu serikali za kaunti. Mgao huo unajumuisha pesa kutoka serikali kuu na washirika wa maendeleo, zikilengwa kusaidia utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo kote nchini. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News