CDC Afrika kuanza kuchapisha data za kila siku za homa ya nyani

  • | BBC Swahili
    2,951 views
    Shirika la afya duniani, WHO linasema huenda mafunzo ya janga la Covid 19 hayatatumika katika kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya homa ya nyani (Mpox) nje ya bara la Afrika. Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika kinaanza kuchapisha data za kila siku kuhusu mlipuko huu. Aina hii mpya imeua mamia ya watu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na imegunduliwa katika nchi nyingine kumi na tano za Afrika. Elizabeth Kazibure anaelezea zaidi ugonjwa huu wa homa ya nyani #bbcswahili #afya #mpox Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw