Chama cha hospitali za kibinafsi, RUPHA chaondoa huduma kwa wanachama wote wa SHA

  • | Citizen TV
    463 views

    Chama cha Hospitali za Kibinafsi RUPHA kimeondoa huduma kwa wanachama wote wa SHA na kampuni ya wasimamizi wa dawa, MAKL. Chama hicho, ambacho kinasimamia zaidi ya vituo 600 vya afya, kinasema hatua hiyo imesababishwa na madeni ya NHIF ambayo serikali imeshindwa kulipa. RUPHA pia inaituhumu MAKL, ambayo inasimamia mipango ya matibabu ya walimu na polisi, kwa unyanyasaji.