Skip to main content
Skip to main content

Chuo Kikuu cha Zetech kimezindua taasisi ya utafiti wa wakongwe

  • | Citizen TV
    343 views
    Duration: 1:39
    Chuo kikuu cha Zetech kimezindua taasisi ya utafiti wa wakongwe kwa ushirikiano na wakfu wa Kinuthia Wamwangi ili kushughulikia changamoto zinazowakabili wazee. Taasisi hiyo itafanya utafiti, kuandaa kambi za matibabu, na huduma za kuwahamasisha umma kuhusu changamoto zinazowakabili wazee. Hatua hiyo inalenga kuimarisha maisha ya wakongwe na kubuni sera za kuwasaidia. Wakongwe pia walipata matibabu ya bure ya macho kwa hisani ya hospitali ya Lions.