'Dada wa Makachu' afukuza umaskini kwa kupiga mbizi baharini

  • | BBC Swahili
    7,928 views
    Je, umewahi kuwazia kujirusha kwenye maji ya kina kirefu kunaweza kuwa ajira inayokuingizia kipato? Sasa Visiwani Zanzibar mchezo maarufu wa Makachu umetoa ajira kwa vijana wengi waliojiwekea nią ya kuzikomboa familia zao kutoka kwenye umaskini, na miongoni mwao ni Albayna Ally anayefahamika sana kama 'Dada wa Makachu' ambaye ni mwanamke pekee anayecheza mchezo huu visiwani humo. Mtangazaji Kinara wa Dira TV Roncliffe Odit alikuwa Visiwani Zanzibar, na kututumia taarifa ifuatayo...