Daktari wa watoto aeleza hospitali pekee ya Nasser imeelemewa na wagonjwa

  • | VOA Swahili
    52 views
    Hospitali Gaza zinakabiliwa na shinikizo kubwa la wagonjwa wengi wanaowapokea na huku huduma zikiwa finyu kutokana na vita. Daktari wa watoto, Mervat Al-Qatati, alisema Hospitali ya Nasser haiwezi kutoa matibabu kwa idadi kubwa ya wagonjwa watoto ambao wanawapokea. Kampeni ya Jeshi la Israel imeziweka hospitali nyingi na vituo vingine vya afya kutoweza kutoa huduma, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), na kusababisha ukosefu mkubwa wa mahitaji ya tiba. Israel inakanusha kukusudia kulenga vituo vya afya au kuzuia upatikanaji wa mahitaji ya tiba kupelekwa Gaza. Vita hiyo ilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji kutoka Palestina wa kikundi cha wanamgambo wa Hamas walipovamia mpakani na kushambulia jamii mbalimbali huko Israel, ikiuwa watu 1,200 na kuwateka watu 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israeli. Shambulizi la Israeli huko Gaza kulipiza kisasi lilianza siku hiyo hiyo kwa kushambulia kwa mabomu na limeendelea kwa miezi tisa pamoja na uvamizi wa ardhini ambapo mamlaka za afya Palestina zinasema imeuwa zaidi ya watu 38,000 na kujeruhi zaidi ya watu 80,000. Idadi kubwa ya waliojeruhiwa kutokana na vita hivyo imeongeza magonjwa kusambaa na utapiamlo kati ya wakati asilimia 90 wa Gaza ambapo Umoja wa Mataifa unasema wamekoseshwa makazi, na kuweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya katika eneo hilo finyu. #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen