EACC yasaka makazi ya gavana Barchok wa Bomet

  • | KBC Video
    501 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC imeanzisha uchunguzi dhidi ya gavana wa Bomet ,Hillary Barchok na maafisa wengine wanane wakuu katika kaunti hiyo kuhusiana na madai ya mkinzano wa kimaslahi na ubadhirifu wa fedha za umma. Uchunguzi huo unaangazia sakata inayohusisha ulipaji wa shilingi bilioni-1.5 kwa huduma ambazo hazikutolewa. Gavana huyo leo asubuhi aliandikisha taarifa katika afisi za tume hiyo jijini Nakuru.Oparesheni ya tume ya EACC iliyofanyika katika kaunti za Nairobi na Bomet, pia iliwalenga wanakandarasi wawili wanaodaiwa kuhusika katika sakata hiyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive