DCI yaanzisha uchunguzi wa madai ya njama ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa kilimo Richard Lesiyampe

  • | Citizen TV
    5,231 views

    Maafisa wa DCI katika kaunti ya Samburu wameanzisha uchunguzi wa madai ya njama ya mauaji ya aliyekuwa Katibu wa wizara ya kilimo Richard Lesiyampe. njama ya kumuangamiza Lesiyampe, ilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii, huku gari lake likivamiwa kwenye barabara kuu ya Maralal kwenda Baragoi wikendi iliyopita. Mwanahabari wetu Bonface Barasa anaarifu zaidi kutoka Samburu.