Douglas Kanja apewa siku 14 kumi na nne kufika mahakamani la sivyo ahukumiwe

  • | K24 Video
    145 views

    Jaji bahati mwamuye wa mahakama kuu amemtahadharisha Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja kwamba atahukumiwa na kufungwa kwa kosa la kudharau mahakama iwapo atakosa kufika mahakamani tarehe 27 mwezi januari, ili atoe maelezo kuhusu uchunguzi unaoendelea kuhusu madai ya utekaji nyara.hii ni baada ya Kanja kukosa kufika mbele ya mahakama hiyo. Katika uamuzi tofauti ,mahakama kuu imeelekeza kuwa aliyekuwa inspekta jenerali wa polisi Japheth Koome anawajibika binafsi kwa hatua za maafisa wa polisi walio mpiga dkt Davji atela wakati wa maandamano ya amani ya madaktari mwaka 2024.