Duale aapa kukabiliana vikali na makundi haramu katika wizara ya afya

  • | KBC Video
    72 views

    Waziri mpya wa afya Aden Duale ameapa kukabiliana vikali na makundi haramu katika wizara ya afya hasa yale yanayohujumu utekelezaji wa bima ya afya ya Jamii-SHA. Duale alifichua kwamba anaungwa mkono kikamilifu na kiongozi wa taifa huku akiapa kukabiliana ipasavyo na mtu yeyote anayejaribu kuhujumu ufanisi wa SHA. Haya yanajiri huku chama cha madaktari nchini-KMPDU kikitoa wito kwa waziri huyo mpya wa afya kujiepusha na siasa anaposhughulikia masuala ya wahudumu wa afya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News