Fahamu jinsi sheria mpya inavyowalinda walemavu Somalia

  • | BBC Swahili
    38 views
    Kwa miongo kadhaa nchini Somalia, watu wenye ulemavu wamekabiliwa na ubaguzi, kutengwa, na ufikiaji mdogo wa haki za kimsingi za Kibinadamu. Asilimia kumi na moja (11%) ya watu wazima nchini humo wana ulemavu, baadhi yao walijeruhiwa wakati wa mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabab wakati wa miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Watu wenye ulemavu wamehangaika kupata ajira, elimu, na kushiriki katika siasa. Hata hivyo, sheria hiyo mpya ya kitaifa ambayo ni ya kihistoria, inalenga kubadilisha taswira hiyo na kuwapa nafasi sawa.