Fahamu kwa nini Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC ametua DRC

  • | BBC Swahili
    4,670 views
    Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imesema itachunguza uhalifu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambapo machafuko ya wiki kadhaa yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine zaidi ya nusu milioni kuyakimbia makazi yao. Mwendesha Mashtaka Mkuu Karim Khan, ambaye kwa sasa yuko Kinshasa, ameelezea wasiwasi wake juu ya mgogoro huo, huku waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiendelea kuteka maeneo na kusonga mbele. Katika ziara yake ya siku mbili, Khan anapanga mikutano na maafisa wa serikali, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na waathiriwa wa vita hivyo.