Familia moja kaunti ya Baringo imeduwazwa na matibabu ya binti yao mdogo

  • | Citizen TV
    466 views

    Huku changamoto za bima ya serikali ya SHA zikiendelea kuripotiwa, familia moja kutoka eneo la Mogotio kaunti ya Baringo inahofia kudorora zaidi kwa afya ya binti yao wa miaka miwili ambaye anaugua maradhi ya Moyo. Mtoto huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji kwa gharama ya shilingi milioni mbili lakini licha ya wazazi wake kusajiliwa katika mpango wa SHA, mtoto huyo hajapata usaidizi.