Familia ya Agnes Wanjiru imekutana na waziri wa Ulinzi wa Uingereza

  • | Citizen TV
    1,853 views

    Familia ya Agnes Wanjiru anayedaiwa kuuawa na mwanajeshi wa Uingereza mwaka wa 2012 sasa inasema italazimika kutafuta haki uingereza iwapo kesi hiyo itakosa kuendelea katika muda wa miezi miwili ijayo. Familia hiyo iliyokutana na waziri wa ulinzi wa Uingereza John Healey hapa Nairobi imeelezea masikitiko ya namna uchunguzi unavyoendeshwa. Haya yamejiri huku mkurungenzi mkuu wa mashtaka Renson Ingonga akisema uchunguzi wa maafisa wa upelelezi umekamilika na maafisa wake wanakamilisha ripoti