Familia zawatafuta waliotekwa bila mafanikio

  • | Citizen TV
    1,847 views

    Takriban wiki moja tangu polisi kuaminika kuwatekwa nyara vijana, familia za vijana hao, zimezidi kukosa usingizi huku juhudi za kuwatafuta zikiambulia patupu. Huku matumaini yao yakiendelea kufifia, familia hizi zinaiomba serikali iwasilishe wana wao mahakamani au kutoa taarifa kuhusu waliko wapendwa wao. Miongoni mwa waliotoweka ni bernard kavuli, billy mwangi, peter muteti, na gideon kibet, ambao wanadaiwa kutekwa nyara muda mfupi baada ya kuchapisha taarifa na picha za kukejeli serikali kwenye mitandao ya kijamii. Na kama anavyoarifu Ben Kirui, licha ya ahadi ya Rais William Ruto hapo jana kuwa atakomesha utekaji nyara, visa hivyo havijakoma.