FKF yahitajika kuchukua hatua za haraka kumaliza vurugu

  • | Citizen TV
    355 views

    Visa vya kushambulia marefarii na kuvunjwa kwa mechi za ligi mbalimbali nchini vimeonekana kuongezeka huku shirikisho la kandanda nchini FKF likihitajika kuchukua hatua za haraka kumaliza uhuni huo. Kisa cha hivi karibuni ni mechi ya supa ligi wikendi iliyopita kati ya 3K FC na Kibera Black Stars uwanjani Moi kaunti ya Embu.