Francis Njuga atafutwa, baada ya kutoweka kijijini Pingilikani

  • | Citizen TV
    484 views

    Familia moja katika kijiji cha Pingilikani eneo bunge la Kilifi Kusini kaunti ya Kilifi imeiomba serikali kuisaidia kubaini aliko jamaa wao ambaye alitoweka tangu mwezi wa Mei mwaka huu. Familia hiyo inasema Francis Chelengeli Njuga, mkulima mdogo, alitoka nje ya nyumba yake kwenda kujisaidia ila hakurudi tena, na kwamba juhudi za kupata usaidizi kutoka kwa mamlaka husika zimeambulia patupu. Familia hiyo sasa inamwomba Waziri wa usalama Kithure Kindiki kusaidia kumpata jamaa huyo aliyetoweka kwani wasimamizi wa eneo hilo wa polisi wameshindwa kufanya hivyo kwa zaidi ya miezi minne tangu kutoweka kwake.