Gavana Dhadho akamatwa kuhusiana na mzozo uliozuka Tana River

  • | KBC Video
    920 views

    Idadi ya watu waliouawa kwenye makabiliano ya kiukoo katika kaunti ya Tana River imeongezeka hadi 18 kufuatia vifo vya watu wanne zaidi katika eneo la Meti. Haya yanajiri huku Inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja akithibitisha kwamba gavana wa Tana River Godhana Dhadho alikamatwa na majasusi wa idara ya upelelezi wa jinai na kuhojiwa kwa saa kadhaa leo kuhusiana na makabiliano hayo. Mwanahabari wetu Fredrick Parsayo anatuarifu zaidi kuhusu kukamatwa kwa gavana huyo hatua ambayo imeshtumiwa na baraza la magavana linalohoji uhalali wa kukamatwa kwake.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive