Gavana Kawira Mwangaza atimuliwa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka miwili

  • | K24 Video
    43 views

    Gavana wa Meru Kawira Mwangaza ametimuliwa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka miwili baada ya wawakilishi wadi 49 kupiga kura kuunga mkono hoja ya kumuondoa afisini. Kati ya wawakilishi wadi 69, 17 walipinga hoja hiyo huku wengine watatu wakikosa kujitokeza kupiga kura. Mwangaza anakabiliwa na madai ya ukiukaji wa katiba, utovu wa nidhamu na matumizi mabaya ya ofisi.