Gavana Mutahi asema kuondolewa kwa Gachagua ni pigo kubwa kwa eneo la kati

  • | KBC Video
    509 views

    Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, anayeaminika kuwa mwandani wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema kuondolewa mamlakani kwa Gachagua ni pigo kubwa kwa eneo la kati mwa nchi, na kwamba eneo hilo litalazimika kuchukua mkondo mpya. Hata hivyo, gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki ameshikilia kuwa Prof Kithure Kindiki ni mzawa wa eneo la mlima Kenya na hivyo eneo hilo linafaa kusalia na umoja. Magavana hao walizungumza wakati wa hafla ya kutoa shukrani iliyoandaliwa na gavana Kahiga, baada ya kuhitimu na shahada ya uzamifu kutoka chuo kikuu cha Kenya Methodist. Magavana wengine waliohudhuria ni pamoja na Stephen Sang wa Nandi, Benjamin Cheboi wa Baringo, na Ken Lusaka wa Bungoma miongoni mwa wengine.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive