Gavana Mwangaza apata afueni baada ya mahakama kuagiza asingatuliwe mamlakani kwa muda wa siku 120

  • | K24 Video
    19 views

    Gavana wa Meru Kawira Mwangaza amepata afueni baada ya mahakama kuu kurefusha maagizo ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi wa bunge la seneti wa kumuondoa mamlakani hadi kesi yake itakaposikizwa na kuamuliwa, hii inamaanisha kwamba mwangaza ataendelea kuhudumu kama gavana wa Meru kwa siku 120 zaidi au hadi uamuzi wa kesi hiyo ufanywe. jaji bahati mwamuye amesema kuondoa maagizo hayo kungesababisha matokeo yenye athari kubwa, na hivyo uamuzi huo umefanywa kwa maslahi ya umma.