"Hii dhana ya kuzuia uchaguzi, utekelezaji wake hauonekani hata kwa tochi"

  • | BBC Swahili
    13,282 views
    Kimeibuka kikundi ndani ya chama kikuu cha upinzani Chadema kinachojiita G-55. Katika siku za hivi karibuni kimeibua mjadala katika mitandao ya kijamii hasa baada ya waraka wao kuibuka ukionesha kupinga mkakati rasmi wa Chadema kuelekea uchaguzi mkuu uitwao ‘No reforms, no elections’. Kundi hili, ambao wanadai wapo zaidi ya watu 55, waliowahi kuwa wagombea ubunge majimbo mbalimbali, watia nia wa ubunge waliopo sasa, wanadai wamepata wito kutoka kwa watia nia wa udiwani wanaotaka kujiunga na kundi. #bbcswahili #chadema #tanzania ThumbnailSubscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw