Hitilafu ya Injini Yasababisha Ajali ya Helikopta Iliyoua Jenerali Ogolla

  • | K24 Video
    753 views

    Ajali ya helikopta ya kijeshi KAF 1501 iliyosababisha kifo cha Mkuu wa KDF Jenerali Francis Ogolla na maafisa wengine tisa mnamo Aprili 8 ilisababishwa na hitilafu katika injini, kwa mujibu wa ripoti ya bodi maalumu ya uchunguzi. Ripoti hiyo ilieleza kuwa helikopta hiyo ilikuwa na sifa ya kutegemewa, lakini haikubaini chanzo halisi cha kuharibika kwa injini hiyo.