Hospitali ya Mediheal mashakani kwa tuhuma za biashara haramu ya uuzaji figo

  • | Citizen TV
    3,879 views

    Hospitali ya Mediheal imejipata mashakani baada ya ripoti ya kamati maalum iliyobuniwa kuchunguza madai ya biashara haramu ya figo kusema kuwa kuna shaka huenda wanahusika na kupendekeza uchunguzi zaidi kufanywa. Kamati hiyo iliyo wajumuisha madaktari, maafisa wa wizara ya afya na wasomi iliibua masuali kuhusu namna hospitali hiyo huendesha utoaji wa figo bila hata kuzingatia uhusiano wa mtoaji na anayepokezwa ambao ni raia wa kigeni. Gatete Njoroge ametuandalia taarifa hii kwa kina