"Huwezi kuyakuta katika eneo lingine lolote hapa Tanzania"

  • | BBC Swahili
    3,816 views
    Huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania unapozungumzia usafiri wa umma 'daladala' ni tofauti na ule uliozoeleka maeneo mengine ya nchi hiyo. Malori ambayo yamegeuzwa matumizi yake, nyuma yakiwa wazi huku abiria wakikaa kwa mtindo wa kutazama ndio usafiri wa umma unaotumika visiwani humo. Ni aina ya usafiri uliowahi kutumika miaka mingi iliyopita Tanzania bara ukifahamika kama 'Chai. maharage'. Mwandishi wa BBC ,Esther Namuhisa alitembelea visiwani Zanzibar nakujionea aina hiyo ya usafiri na kuandaa taarifa hii.#usafiriwaumma